Kwa maudhui

Vivumishi ni maneno yaliyowekwa kabla ya kundi nomino ili utambulisho wake ufafanuke. Mfafanuzi muhimu zaidi ni kifungu cha kufafanua la .

La-kibainishi wazi

Neno la linaonyesha kwamba tunazungumzia ya kitu kinachojulikana kwa msikilizaji .

Hauongezi mwisho kwa la, si J wala N:

  • la domo = ni nyumba inayojulikana kwako
  • la bela junulino = msichana mrembo anayejulikana kwako
  • la junulinoj = wasichana wanaojulikana kwako
  • la altaj montoj = milima mirefu inayojulikana kwako
  • la ruĝajn krajonojn = penseli nyekundu zinazojulikana kwako

Kwenye mazingira fulani unaweza kutumia mfumo wa apostrofi iliyofupishwa l'

La inasimama kabla ya wasifu nyingine ya nomino. Inawezekana kihusishi kimewekwa kabla ya la:

  • en la domo
  • ĉe la bela junulino
  • pri la altaj domoj

vitu binafsi

Linapokuja suala la watu binafsi (si kuhusu aina ), la inamaanisha kwamba msemaji anadhani kuwa msemaji anajua jambo hilo. la kisha inamaanisha kwamba kwa namna hii ama nyingine "unajua kile ninachozungumzia."

Ukosefu wa la (au ufafanuzi mwingine) inamaanisha kwamba msemaji anafikiri kwamba msikilizaji hajui kitu. Ukosefu wa kivumishi unamaanisha kwa namna hii au nyingine "hujui kile ninachozungumzia." Ukosefu wa kivumishi pia unaweza kumaanisha kuwa utambulisho haujalishi. Kutotumia la ni muhimu kama kuitumia la .

  • La rozo apartenas al Teodoro. - Rose ni ya Teodore.

    Msemaji anafikiri kwamba msikilizaji anaweza kuelewa ni rose gani inayolengwa.

  • Al Teodoro apartenas rozo. - Rose ni ya Teodore.

    Sasa ni rose ambayo msikilizaji hajui.

  • Domo brulas! - Nyumba huwaka!

    Nyumba huwaka, lakini msemaji hajui kama msikilizaji anajua ni nyumba, au labda msemaji hajui hata nyumba inayowaka

  • La domo brulas! - Ile nyumba inawaka!

    Msemaji anataka kuwajulisha kuwa nyumba ambayo msikilizaji anatakiwa kujua (labda nyumba yake) inawaka.

  • Venis multaj gastoj al via festo, ĉu ne? - Wageni wengi wamekuja kwenye sikukuu yako, kweli?

    Wageni walikuwa kweli watu wanaojulikana, lakini hapa maneno multaj gastoj hutumikia tu kuwajulisha idadi ya wageni. Utambulisho wao binafsi au kikundi haujalishi.

Imetajwa hapo awali

Kwa kawaida kitu kinajulikana, kwani kimesemwa hapo awali. La kipindi hicho ina maana kwamba wamesema tena kitu ambachokimetajwa. Kuondoa la inamaanisha kuwa kitu kipya kinapatikana katika dibaji:

  • Mi havas grandan domon. La domo havas du etaĝojn. - Nina nyumba kubwa. Nyumba ina sakafu mbili.

    Wakati wa kwanza msikilizaji hajui ni nyumba gani. Kwa hiyo msemaji hatumii la. Wakati wa pili kutaja msemaji anaongezea la kwa kuonyesha kuwa ni nyumba iliyosemwa awali. Ikiwa hakutumia la basi, msikilizaji atadhani kwamba ni nyumba nyingine tofauti na ile ambayo ilitajwa au juu ya nyumba kwa ujumla (nyumba yoyote).

  • En tiu ĉi skatolo estas frukto. La frukto estas ronda. - Katika sanduku hili kuna matunda. Matunda hilo ni la mviringo.

    Kwanza frukto (bila la) inaleta suala jipya. Msikilizaji anajua kwamba kuna tunda katika sanduku. Kisha msemaji anaweza kuendelea kusema kuhusu matunda akitumia maneno la frukto. (tunda)

  • Mi havas tri infanojn. La infanoj ofte ĝojigas min. - Nina watoto watatu. Mara nyingi watoto hunifanya niwe na furaha.

    La inaonyesha kwamba ni watoto waliojajwa hapo awali.

  • Sur la strato iris tri viroj. Ili aspektis kiel friponoj. Subite la tri friponoj malaperis en bankon. Ŝajnis, ke la banko estas prirabota. - Wanaume watatu walikwenda barabarani. Walionekana kama machizi. Ghafla wale machizi watatu walipoteleya ndani ya benki. Benki hiyo ilionekana kuwa itaibiwa.

    Baada ya kutaja kwanza wanaume watatu, kwamba wanaonekana kama machizi, unaweza kuwaita tu la (tri) friponoj (tatu). Sehemu ya sentensi la tri friponoj hutumika jina la kibinafsi la ao wanaume watatu. Baada ya kutaja kwanza benki, uinaweza kuiita la benko.

Sio lazima kutumia maneno ya kufanana ili uweze kuzungumza jambo moja na la:

  • Tre malproksime de ĉi tie loĝis reĝo, kiu havis dek unu filojn kaj unu filinon, Elizon. La dek unu fratoj iradis en la lernejon kun stelo sur la brusto kaj sabro ĉe la flanko. - Mbali sana na hapa paliishi mfalme ambaye alikuwa na watoto kumi na moja na binti moja, Elizo. Awo dugu kumi na moja walienda shule na nyota kwenye kifua na upanga pembeni.

    Ingawa kwanza walitajwa kwa neno foj, basi wanaweza kuwaita la dek unu fratoj (kumi na moja).

Haijatajwa moja kwa moja, vipawa,ina kisika

Mara nyingi kuna kitu kinajulikana kwa sababu kitu kingine kinachoelezwa hapo awali kinaweka hazarani kuwepo kwake, au kwa sababu msikilizaji ana habari za kutosha kuhusu ilo jambo:

  • Mi aĉetis aŭton, sed la motoro ne funkcias. - Nilinunua gari, lakini injini haikufanya kazi.

    Injini yenyewe haijaelezewa moja kwa moja kabla, gari pekee, gari tu, ila kwa sababu kila gari lina injini, msikilizaji anaweza kuelewa kwamba ni injini ya gari lililotajwa hapo awali. Mtu anaweza pia kusema injini yake, ambayo itakuwa wazi zaidi.

  • Mi manĝas per la buŝo kaj flaras per la nazo. - Ninakula kwa kinywa na usa kwa pua.

    Msikilizaji anajua kwamba msemaji ni mtu, na kwamba mtu ana mdomo na pua. kinywa na pua vinafanana na kinywa changu na pua yangu . Inawezekana kuondoa la, lakini ingeweza kusikia kidogo kama msemaji alisita kuwa msikilizaji anajua kwamba mtu ana mdomo na pua.

Imeelezwa kikamilifu

Sehemu ya sentensi inaweza kuwa na wasifu au nyongezo ambayo inaeleza zaidi:

  • Jen kuŝas la ĉapelo de la patro. - Ona kofia ya baba ilipo.

    Wasifude la patro (ya baba) inaeleza ni kofia gani. Mtu anaelewa kuwa baba ana kofia moja tu. Ikiwa mtu hakutumii la , basi ni lazima ujuwe kuwa ni kofia moja miongoni mwa kofia kadhaa za baba.

  • Por la hodiaŭa tago mi ricevis duoblan pagon. - Kwa siku ya leo nilipokea malipo mara mbili.

    Wasifu hodiaŭa inafafanua kikamilifu siku gani.

  • Mi redonas al vi la monon, kiun vi pruntis al mi. - Ninakupa pesa uliyonipa.

    Sehemu kiun vi pruntis al mi inafafanua kikamilifu ni pesa gani.

  • Mi vojaĝis al la urbo Pekino. - Nilienda mjini Beijing.

    Jina Beijing linafafanua kikamilifu mji.

Kinachoonekana moja kwa moja

Jambo linaweza kujulikana kwa sababu msikilizaji anaiona moja kwa moja, au labda anaelewa:

  • La domo estas vere bela. - Kiuhakika nyumba hiyo ni nzuri.

    Hivyo, mtu anaweza kusema wakati wajumbe wanaona nyumba.

  • La floroj odoras tre bone. - Maua hanukia vizuri.

    Kwa hivyo inawezekana kusema wakati msikilizaji mwenyewe anaona au anasikiya rehe ya maua maua.

Inajulikana kwa ujumla kuwa ni pekee

Kitu kinaweza kujulikana kwa sababu ni cha kipekee kabisa, kwa sababu tu ni kitu kimoja, au kwa sababu pekee yake kinaweza kungelewa tu:

  • La ĉielo estas blua. - Anga ni la bluu.

    Kila mtu anajua kwamba anga lipo. Kwa hivyo linaweza kuitwa, tu, la ĉielo (anga).

  • La prezidanto de Usono diris, ke... - Rais wa Amerika amesema kwamba....

    Msemajianapaswa kwamba msikilizaji anajua kwamba Marekani ina rais, na ni mmoja tu. Kwa hiyo, inawezekana tu kumuita la prezidento de Usono

Aina

Mara nyingi nomino inatumiwa kuzungumza juu ya aina, aina, ili useme kia (aina gani) ni. Hii inaweza kufanyika kwa njia mbalimbali: bila la, pamoja na la, ikiwa mu umoja au mu wingi. Mara nyingi inaweza kutumika katika namna yoyote kulingana na mtindo.

Mara nyingi huwa hutumiwa wakati wa kuzungumza kuhusu aina, aina. Ni kama kuchukuliya aina fulani moja asiyojulikana, au kama mtu ambaye utambulisho wake wauhitajiki sana.

  • Leono estas besto. - simba ni mnyama.

    Unaweza kusema,kwamba simba ni moja ya aina ya minyama,siyo mmea au kitu kingine.

  • Rozo estas floro kaj kolombo estas birdo. - Rose ni maua na njiwa ni ndege.

    Ni makundi,siyo binafsi.

  • Karlo estas kuracisto. - Charles ni mganga.

    Nenokuracisto halitambulishi lakini linasema kazi gani Charles anayo.

  • Elizabeto estas patrino de tri infanoj. - Elizabeth ni mama wa watoto watatu

    Sentensipatrino de triinfano hutumiwi kwa kuonyesha Elizabeth ni nani, lakini kutuambia ni mtu aina gani.

  • Akvo bolas je cent gradoj. - Maji huchemka kwa kiwango cha joto la degree 100.

    Hawazungumzii juu ya mkusanyiko fulani wa maji, lakini juu ya dutu kwa ujumla.

Wakati mwingine tunaangalia aina ambayo kitu kinachojulikana, na kinatumia la. Hii ni ya kawaida katika mtindo wa falsafa. Katika matukio hayo yanalenga aina yote:

  • La gitaro estas tre populara instrumento. - Gitaa ni kifaa maarufu sana.

    Wanesema aina ya chombo kama ni chombo ambachokinajulikana bila shaka . Uwezekano mwingine ni: Gitaro estas...

  • La kato preferas varman klimaton. - paka hupenda wakati wa joto

    Wanasema aina ya mnyama kama mnyama mmoja aliyejulikana. Unaweza pia kusema: Kato preferas...

  • La urso troviĝas kaj en Eŭropo kaj en Ameriko. - dubu hupatikana pote Ulaya na Amerika.

    Yanayosemwa hayana maana kwa dubu moja tu. Kwa hivyo mtu hawezi kusema: Urso troviĝas kaj en Eŭropo kaj en Ameriko.

  • La saĝulo havas siajn okulojn en la kapo, kaj la malsaĝulo iras en mallumo. La saĝulo = ĉiuj saĝuloj. La malsaĝulo = ĉiuj malsaĝuloj. - Mwenye hekima ana macho yake kichwani, na mpumbavu huenda gizani. Mtu mwenye hekima = watu wote wenye hekima. Mpumbavu = wapumbavu wote.

Ikiwa nomino linatumiwa kama prediketo, basi hakikisha usitumie la, ikiwa tunazungumza tu juu ya kikundi: Karlo estas advokato. Ikiwa tunasema Karlo estas la advokato, basi maana ni "Karlo ni hakimu fulani ambaye unajua "au" Karlo ni mwanasheria huyu ambaye tunazungumzia "au kama hivo.

Ikiwa tunataja jambo linaloweza kuhesabika, basi tunaweza pia kuwakilisha aina au jamii kwa neno la wingi. Wakati wa kuzungumza juu ya aina tofauti kati ya umoja na wingi mara nyingi haiitajiki:

  • Leonoj estas bestoj. = Leono estas besto.
  • Rozoj estas floroj kaj kolomboj estas birdoj.
  • La leonoj estas bestoj.
  • La rozoj estas floroj kaj la kolomboj estas birdoj.

Uzuiaji wa la

Usitumie la kwa kipengele cha sentensi ambacho tayari kina kitambulisho kingine. Vitambulisho ni Viwakilishi vimilikishi , correlative yanayoishia na U, A au ES, tumaneno vyote viwili au wawili, na kitambulisho cha sehemu unu } :

  • Mia dorso doloras. - Mgongo wangu una maumivu.

    Siyo:La mia dorso doloras.lakini inawezekana la mia/via...,kama haifuatwi na nomino.)

  • Tiu domo estas granda. - Ile nyumba ni kubwa

    Siyo: La tiu domo estas granda.

  • Ĉiuj gastoj jam venis. - Wageni wote wameshakuja.

    Siyo:Ĉiuj la gastoj jam venis.wala:La ĉiuj gastoj jam venis.

  • Mi ŝatas ĉiajn legomojn. - napenda aina zote za mbogamboga.

    Hapana:Mi ŝatas la ĉiajn legomojn.

  • Kies gasto mi estas, ties feston mi festas. - Nikiwa mgeni wa vmtu, sikukuu yake naisherehekeya.

    Si:La kies gasto... la ties festo...

  • Mi legis ambaŭ librojn. - Nimesoma vitabu vyote viwili.

    Si:Mi legis la ambaŭ librojn.wala:Mi legis ambaŭ la librojn.

Usitumielakabla yavocative:

  • Kelnero, alportu al mi glason da biero! - Muhudumu, niletee glasi bia!

    Usiseme:La kelnero, alportu...

Labadala ya kiwakilishi kimilikishi

Neno la linatumiwa mara nyingi badala ya Viwakilishi vimilikishi(4), ikiwa mazingira yanaonyesha wazi mmiliki. Hii hutokea mara nyingi hasa wakati wa kuzungumza kuhusu jamaa na sehemu za mwili:

  • Li levis la kapon. = Li levis sian kapon. - Akainua kichwa=Akainua kichwa chake.
  • Mi montris per la fingro, kien li iru. = ...per mia fingro... - Nilionyesha kwa kidole ambapo anapaswa kwenda.=kidole changu....
  • Ŝi lavis al si la piedojn. = Ŝi lavis siajn piedojn. - Aliosha miguu yake yeyemwenyewe.=Aliosha miguu yake.
  • Ĉu Karlo venis kun la patro? = ...kun sia patro? - Karlo aliweza kuja na baba yake?=...pamoja na baba yake mzazi?
  • Diru al la patro, ke mi estas diligenta. La patro = mia patro (la patro de la parolanto)
    - Mwambie baba kwamba ninaongoza.Baba=baba yangu(baba wa mzungumzaji).

    Hata hivyo, mara nyingi maneno Patro na Patrino (pamoja na herufi kubwa ya kwanza) kama majina binafsi hutumiwa bila la

LaLabadala ya ĉiujĉiuj{4}

Wakati hakuna nafasi ya kutokuelewana unaweza kutumia la badala ya ĉiuj :

  • La gastoj eksidis ĉe la tablo.Ĉiuj gastoj eksidis... - Wageni walichukua nafasi mezani.≈Wageni wote walichukua nafasi zao.....
  • Ĉi-vespere la Angloj prezentos teatraĵon en la kongresejo. La Anglojĉiuj Angloj. - Jioni hii Waiingereza watacheza kwenye ukumbi wa muhadhara. Waingereza ≈ Waingereza wote.

    Hali (mkutano) hata hivyo inaweka maana ya ĉiuj Angloj . Tunazungumzia juu ya (kwa namna hii ama nyingine) waiingereza wote wanaoshiriki katika mkutano, na sio kuhusu Waingereza wote duniani.

Lakabla majina ya lugha

La hutumiwa kabla ya majina ya lugha ambayo yanajumuisha vivumishi na neno lingvo (lugha). La hutumiwa kwa sababu lugha huonekana kuwa ya kipekee: la Angla (lingvo), la Ĉina (lingvo), la Nederlanda (lingvo) nk Lakini la haipaswi kutumiwa kwa majina ya lugha chache ambazo zina jina kama nomino Esperanto, Sanskrito, Ido, Volapuko nk

Lakabla ya plej na malpej

Kipindi plej au malplej zipo, kwa kawaida tunazungumzia juu ya jambo la kipekee, na unatumia la:

  • La malfeliĉa infano forkuris kaj kaŝis sin en la plej proksima arbaro. - Mtoto masikini alikimbia na alijificha katika msitu wa karibu.
  • Li estas tre kredema: eĉ la plej nekredeblajn aferojn, kiujn rakontas al li la plej nekredindaj homoj, li tuj kredas. - Yeye anaamini sana: hata vitu ambavyo huezi kuamini ambavyo waongo wanamusimulia, yeye anakubali.

Wakati wa kufananisha vitu viwili au vikundi viwili basi tunatumia maranyingi la (mal) pli badala ya la (mal) plej:

  • Unu vidvino havis du filinojn. La pli maljuna [filino] estis tiel simila al la patrino per sia karaktero kaj vizaĝo, ke ĉiu, kiu ŝin vidis, povis pensi, ke li vidas la patrinon. - Mjane mmoja alikuwa na binti wawili. Mwanamke mkubwa (binti) alimfana mama yake katika tabia na uso wake, kwamba kila mtu aliyemwona anaweza kufikiri kwamba alimwona mama.

Wakati mwingine plej haiakilishi kitu cha kipekee, lakini huonyesha kiwango cha juu cha ubora au namna. Katika hali hiyo usitumie la :

  • vulpo plej ruza fine estas kaptata. - Hata mbweha mjanja alikamatwa mwishoni.

    Hatuzungumzii juu ya mbweha fulani inayojulikana, lakini kuhusu mbweha yoyote ambayo ni mjanja sana.

  • Li estas plej laca en la mateno. - Yeye anachoka sana asubuhi.

    Hii siyo kulinganisha watu tofauti, lakini kulinganisha aina tofauti za uchovu wa mtu mmoja baada ya muda.

  • Kiu venas plej frue, sidas plej ĝue. - Anayefika mapema hukaa pazuri.

    Plej haisimami mbele ya jina la kipengele cha sentensi lakini mbele ya kielezi kipengele cha sentensi.

Lana majina ya kipekee

Usitumie la kwa maneno ambayo ni majina ya pekee (majina), kwa sababu majina haya yanajieleza yenyewe:

  • Pasintjare mi vojaĝis al Kanado. - Mwaka jana nilisafiri Canada.

    Usiseme: ...al la Kanado.

  • Kie estas Francisko? - Francisko yuko wapi? (Au Francisko ni wapi)

    Usiseme:Kie estas la Francisko?

Kwa maneno ya kawaida ambayo huja kuwa majina yapekee kwa kawaida tunayatumia la kwa sababu maneno hayo hayajielezi yenyewe.

  • Kaj tiam la Nokto diris: "Tenu vin dekstre kaj eniru en la malluman pinarbaron, mi vidis, ke tien foriris la Morto kun via malgranda infano." - Na usiku Ulisema: "Endelea kulia na uende kwenye msitu wa giza wa msohobari. Niliona Kifo kilikwenda pale na mtoto wako mdogo."

    Katika hadithi, usiku na kifo huwa na jukumu la watu vikiwa na majina yapekee (yaliyoonyeshwa na herufi kubwa), lakini nokto na morto ni majina ya kawaida nkwa hiyo yanahitaji la

Wakati jina la kawaida liko na kivumishi kama wasifu, na ikiwa kivumishi hiki sio sehemu ya jina la pekee, kwa kawaida tunatumia la . Hii inafanywa hasa wakati kuna uchaguzi (halisi au kufikiria) kati ya mambo kadhaa na jina hilo hilo:

  • Duoble montriĝis la bildo de Venero, de la surtera Venero. - Huonyeshwa kipande cha picha ya Venus, ya Venus wa duniani.

    Venus ni jina pekee la mungu wa kike. Kwanza Venero huonekana bila la kulingana na sheria za msingi kwa majina ya kawaida. Kisha tuna wasifu wa duniani na tunapaswa kutumia la ili kuonyesha ubainisho. Ni kama kuna Venus wawili tofauti, Venus wa mbinguni na Venus wa duniani.

  • Ĉiuj konas Londonon, la ĉefurbon de Britio, sed ne ĉiuj konas la aliajn Londonojn en Usono kaj Kanado. - Kila mtu anajua London, mji mkuu wa Uingereza, lakini si kila mtu anajua London nyingine nchini Marekani na Canada.

    Londono (London) haina la . Maonyesho aliaj Londonoj (zingine Londons), hata hivyo ina wasifu aliaj (nyingine), na kwa hiyo anapata neno la .

  • Multaj vizitis Londonon, la ĉefurbon de Britio, sed mi vizitis ankaŭ aliajn Londonojn. - Wengi wametembelea London, mji mkuu wa Uingeleza, lakini pia nilitembelea zingine London.

    Hapa pia Londono ina wasifu, lakini hatutumii la kwa sababu sio zingine London, na msikilizaji pia hawezi kujua kwa usahihi ni London gani tunazungumzia.

Vibainishi vingine zaidi ya la vinaweza kuonekana kabla ya aina yoyote ya jina pekee, lakini si maranyingi misemo hiyo inahitajika..

  • Ha, tie vi estas, mia Elizabeto! - Ah,upo hapo,Elizabeth wangu!
  • Ĉu vi sentas teruron antaŭ tiu Karolo? - Je ,unaogopa Karolo?

Kibainisho cha nusu unu

Lugha zingine hutumia vibainisho visivyokuwa wazi, ambavyo mara nyingi ni neno sawa na nambari unu (moja). Vibainisho visivyokuwa wazi katika lugha ya Kiesperanto havipo. Ukikataa kuweka wazi unaamua kuacha kibainishi Lakini maramoja maramoja unaweza kutumia unu kama duondifinan artikolon. (kibainisho cha nusu). Matumizi haya ya unu hainyeshi namba, bali ni ya kibinafsi. Inaonyesha kwamba tunazungumzia kitu ambacho haijulikani kwa msikilizaji, lakini kinajulikana kwa msemaji :

  • Unu vidvino havis du filinojn. - Mjane mmoja ana mabinti wawili.

    Mwanzo wa hadithi. Hata na ivi msimuliaji peke yake amjuwa uyo mjane.

  • Unu vesperon fariĝis granda uragano. - Siku moja jioni kulikuwa na kimbunga kikubwa.

Kibainishi unu , hata hivyo, si lazima kitumiwe. yanaongeza nuance, kinaweza kutumika kulingana na mahitaji.

Kurudi juu